MMILIKI WA SHULE YA SEKONDARI YA SCOLASTICA ASOMEWA SHTAKA LA MAUAJI


Anayetajwa kuwa mmiliki wa shule ya Sekondari ya Scolastica,Edward Shayo akijiandaa kuingia chumba cha mahakama.

Anayetajwa kuwa mmiliki wa shule ya Sekondari ya Scolastica iliyopo mji ndogo wa Himo ,Edward Shayo na wenzake wawili ,Hamid Chacha ,Laban Nabiswa wakisindikizwa kuingia chumba cha mahakama.
Anayetajwa kuwa mmiliki wa Shule ya Sekondari ya Scolastica ,Edward Shayo na wenzake wawili wakitoka nje ya chumba cha mahakama mara baada ya kusomewa shtaka la kuua kwa kukusudia.
Mmoja wa ndugu wa kijana Humphrey Shayo akikia kwa uchungu wakati akitoka katika chumba cha mahakama
Ndugu wa anayetajwa kuwa mmilikiwa wa shule ya Sekondari ya Scolastica,Edward Shayo wakionekana kwenye huzuni mara baada kusomewa kwa mashtaka ya mauaji kwa ndugu yao hiyo.
**
WATUHUMIWA watatu kati ya 11 wanao shikiliwa na jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za mauaji ya Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Scolastica ,Humphrey Makundi wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ,Moshi na kusomewa shtaka la mauaji .

Washitakiwa wawili ,Hamis Chacha aliyekuwa mlinzi wa shule ya Skolastica na Labani Nabiswa walifikishwa mahakamani hapo wakitokea kituo kikuu cha kati cha Polisi wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Polisi wenye silaha .

Baada ya Nusu saa Mmiliki wa shule ya Scolastica ,Edward Shayo alifikishwa mahakamani hapo na askari Kanzu akitokea Hostali ya Rufaa ya KCMC alipokuwa akipatiwa matibabu ya baada ya kupata tatizo la kiafya tangu kushikiliwa kwake.

Upande wa Jamhuri katika shtaka hilo lililofika mbele ya Hakimu Mkazi ,Julieti Mawore umewakilishwa na Mwanasheria Kassim Nassiri akisaidiana na Wakili wa kujitegemea ,Faygrace Sadallah huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Eliakunda Kipoko anyemtetea Mshatakiwa wa pili katika shtaka hilo Edward Shayo.

Akisoma maelezo ya hati ya mashtaka mbele ya mahakama hiyo ,Nassiri alieleza kuwa mnamo Novemba 6 mwaka huu mshtakiwa wa kwanza ,Hamis Chacha(28),wa pili Edward Shayo (63)  na wa tatu Laban Nabiswa (37) walimuua kwa kukusudia mtu aitwaye Humphrey Makundi.

Kutokana na maelezo hayo Hakimu ,Mawore alieleza kuwa washtakuwa hawaruhusiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikliza shtaka la mauaji huku akiwataka kungojea kufanya hivyo pindi watakapofikishwa mahakama kuu ambapo watapata nafasi ya kuwasilisha mashahidi wao pamoja na kujitetea.

Kuhusu upelelezi wa Shtaka hilo Mwanasheria wa serikali Nassiri aliieleza mahakama kuwa upelelezi haujakamilika huku akiwasilisha ombi la kupangwa tarehe nyingine kwa ajili kutajwa kwa shauri hilo wakati upelelezi ukikamilishwa.

Hakimu Mkazi ,Mawore aliahairisha shtaka hilo na kupanga kutajwa kwa shtaka hilo Desemba 8 mwaka huu  na  kwamba washtakiwa wote watarudishwa Rumande kutokana na  kesi hiyo kutokuwa na dhamana .

Washatakiwa hao wamefikishwa mahakamani zikiwa  zimepita siku 11 tangu kufukuliwa kwa mwili wa mtu aliyezikwa na Halmashauri ya Manspaa ya Moshi kuondoa utata wa kupotea kwa Mwanafunzi Humphrey Makundi (16) aliyekuwa anasoma shule ya sekondari ya Scolastica iliyopo mji mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro.
Imeandikwa na Dixon Busagaga wa globu ya jamii ,kanda ya Kaskazini.
Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment