Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Novemba, 2017 amemjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu anayepata matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
Mhe. Samia Suluhu Hassan amemfikishia salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amemtakia matibabu mema na kupona haraka ili arejee nyumbani na kuendelea na majukumu yake.
Mhe. Tundu Lissu amemshukuru Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumjulia hali na amewatakia heri katika majukumu yao.
“Msalimu Mhe. Rais mwambie namshukuru sana kwa salamu zake na kunijulia hali” amesema Mhe. Tundu Lissu.
0 comments:
Post a Comment