MTU Mmoja amekufa na wengine saba kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne likiwemo lori lililogonga basi mali ya kampuni ya Johanvia Express lililokuwa likitoka Musoma mkoani Mara kuelekea Dar es Salaam.
Askari wa ukosi cha usalama Morogoro wamebainisha kubwa lori la mafuta lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Morogoro liliiparamia basi hiyo majira ya saa 5 usiku wa Juni 18 katika eneo la Kingolwira, barabara ya Morogoro - Dar es Salaam, Manispaa ya Morogoro.
Imediawa kabla ya kutokea kwa ajali hiyo lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T 883 DMA likiwa limebeba matenga ya nyanya na likitokea Iringa kuekea Dar es Salaam lilipata hitilafu ya kukatika propera na kupoteza uelekeo kabla ya kupinduka katika eneo hilo.
Wakati inatokea ajali ya basi na Lori la mafuta, Askari wa Kikosi cha usalama barabara walikuwa kiwahudumia majeruhi wa Fuso na dakika chache itakotokea ajali hiyo ya basi na Lori na hivyo kuzua taharuki eneo hilo ambapo njia kuu ya Morogoro - Dar es Salaam iliziba kwa saa kadhaa.
Una maoni usisite kutuandikia
KapolanewsUpdates ✍️
0 comments:
Post a Comment