WATU 25 WAMENUSULIKA KUFA BAADA YA KUNYWA POMBE YENYE SUMU MKOANI SONGWE.


Taharuki imeibuka katika Kijiji cha Halambo Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe baada ya watu 25 kufikishwa katika hospitali ya wilaya hiyo kwa madai ya kuugua baada ya kunywa pombe ya kienyeji.

Inadaiwa watu hao walikunywa pombe hiyo sehemu moja ambapo baadae walianza kuumwa tumbo na kuhara na walipatiwa huduma ya kwanza katika zahanati ya kijiji hicho.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Halambo, Lazima Mwambani amesema siku ya tukio hilo Ijumaa Juni 2, 2023 kulikuwa na msiba kijijini hapo ambapo baada ya mazishi watu walienda kunywa pombe kilabuni hapo.

"Tukio hilo lilitokea Juni 2 mwaka huu na idadi ya walioathirika ni watu 31 ambapo baadhi yao walipata madhara siku hiyohiyo lakini wengine walianza kuumwa siku iliyofuata" amesema Mwambani.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Dk Nelson Mponjoli amesema aliwapokea watu 25 ambao walitibiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani kwao.

"Siwezi kuthibitisha kama walikunywa kinywaji chenye sumu ninachoweza kusema watu 25 walifikishwa hospitalini wakiwa wanasumbiliwa na kuhara na tumbo kuuma, hata hivyo hali zao hazikuwa mbaya walitibiwa na kuruhusiwa kurudi," amesema Mponjoli

KapolanewsUpdates ✍️
Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment