Wakazi wa kata ya Tandika Manispaa ya Mtwara Mikindani wameiomba Serikali kuwasaidia kusafisha eneo la Makaburi Msafa ili kudhibiti vitendo vya wizi pamoja na watu kugeuza eneo hilo kuwa sehemu ya kufanyia mapenzi wakati wa usiku.
Akizungumza na Mwandishi wa habari mtaani hapo, Zamda Meza mkazi wa Tandika amesema licha ya kuwa na kipori ambacho hugeuzwa ‘gesti bubu’ lakini kumekuwa na vibaka ambao hutumia eneo hilo na kusababisha watu kushindwa kupita usiku.
“Hili eneo la makaburi lina majani mengi ambayo yanatunza watu wabaya hivyo kuwa tishio kwa wanawake na watoto hasa wakati wa usiku yaani eneo hili makaburi hayaheshimiki watu wemegeuza ‘gesti bubu’ afadhali uwekwe utaratibu wa kufanya usafi wa mara kwa mara” amesema Zamda.
0 comments:
Post a Comment