Kwa taarifa yako…tunakoelekea, wadudu watakuwa miongoni mwa kitoweo bora zaidi kuliko baadhi ya vitoweo kama vile nyama ya ngombe, mbuzi hata kuku. Hii inaweza kuwa fursa nzuri tu ya biashara…jipange. 😋😋😋
Tafiti zinaonesha kuna zaidi ya aina 2000 za wadudu ambao wanaweza kuliwa duniani. Baadhi ya wanaoliwa ni pamoja na mende, viwavi, nyuki, nyigu, nzige, kumbikumbi, senene, nge, vipepeo, kerengende na wengine wengi.
Wajuzi wa mambo wanasema
• Takribani asilimia 80 ya mwili wa mdudu umeumbwa na protini na virutubisho, ambapo protini yake inazidi ile ya mnyama afugwaye.
• Wadudu wana kiwango kidogo cha mafuta, wanga na wamesheheni vitamini, madini na kamba kamba (fibres).
• Minyoo nayo ina kiwango sawa cha Omega-3 kama kwenye samaki.
• Wadudu hawaambukizi magonjwa kwa binadamu na wanyama kama ilivyo kwa wanyama.
Chaguo ni lako jirani…kumeza au kutema
KapolanewsUpdates ✍️
0 comments:
Post a Comment