Jeshi la Polisi jimbo la Edo nchini Nigeria, linamshikilia mtu mmoja Okhiria Eze akituhumiwa kumpiga risasi mkewe mbele ya mtoto wao mdogo, kufuatia mabishano ya kuchelewa kumuandalia chakula.
Kamanda wa Polisi wa Edo, Chidi Nwabuzor amesema tukio hilo lilitokea Juni 3, 2023 katika jamii ya Ekae, eneo la New Etete, GRA, lililopo mtaa wa Benin na idara ya Polisi ya New Etete ikipokea malalamiko hayo toka kwa wazee wa eneo la Ekae.
Amesema, “mshukiwa alibishana vikali na mkewe kwa sababu alichelewa kuandaa chakula chake, baadaye alikwenda kuchukua bunduki yake na kumfyatulia risasi na kusababisha risasi kumpiga mkono wa kushoto.”
Aidha, mbele ya Waandishi wa Habari Kamanda Nwabuzor amesema majeraha ya risasi hiyo yalipelekea mwanamke huyo, Tina Okhiria kukatwa mkono, huku mtoto wa mdogo Joanki Okhiria (9), akikiri kushuhudia mzozo baina ya wazazi wake.
KapolanewsUpdates ✍️
0 comments:
Post a Comment