Kishimba ameyasema hayo wakati akifanyiwa mahojiano na Dar24 Media ambapo ameeleza sababu za kuchangia bungeni na kutaka mtaala wa elimu ubadilishwe.
‘’Kwakweli katika kitu ambacho kilikuwa kinaniumza sana kishwa ni elimu maana mimi mwenyewe ninawatoto najua ile shida ambayo nimepata wanadegree wengine wana Masters yani unamuona mtu kabisa huyu kwa kazi yake, peke yake hawezi’’.‘
’Alifundishwa akasoma lakini ukimuangalia unaona kabisa kuna vitu vingi sana anakosa pamoja na kwamba ameenda muda mrefu darasabi ndio maana mara kwa mara bungeni tumekuwa tukivutana’’
Amesema kuwa ’’tunafanya mabadiliko lakini mimi rohoni bado nilipenda mtu afundishwe kutafuta pesa akiwa darasa la kwanza kwasababu mzungu yeye aliposema kwamba wewe usome ufuate utaratibu huu ilikuwa akuajiri wewe lakini sasa hivi hakuna ajira’’ amesema Kishimba.
Aidha ameongeza kuwa ‘’mtoto wadarasa la kwanza usipomfundisho kwamba kitu hiki huwa kinakuwa hivi akaju madhara yake yatakuwa nini? maana yake hata ukikataa, mtoto asubuhi akiamka anaomba hela ya biskuti anaomba hela ya soda je? ukimfundisha yeye kutafuta hela ya soda kutakuwa na ubaya gani na je akijua hela madhara yake huwa nini? madhara yake atakuwa tu mfanyabishara au atatunza hela kuliko sasa hivi kukataa kabisa asifundishwe mtoto hela lakini afundishwe kuomba hela na kula hela’’
Amesema kuwa, mfano wa Nchi ya Libya ambayo ilikuwa ni nchi tajiri kabla ya kuingia kwenye machafuko ambapo amesema kuwa nchi nyingine yenye utajiri ni Botswana na kusema kuwa raia wake wanachunga ngombe na ndiyo nchi yennye pesa nyingi.
KapolanewsUpdates ✍️
0 comments:
Post a Comment