Nchi 10 duniani zenye majengo mazuri ya Ikulu, mbili zipo Afrika

Ni kawaida majengo mengi ya IKULU duniani kujengwa kwa namna za kipekee na kuvutia kwa sababu hutumika kama Ofisi na makazi ya Marasi wa nchi, Wafalme na Malkia, sasa leo April 8, 2017 nimekutana na list ya majengo 10 mazuri ya IKULU duniani.

1: Washington, Marekani
Ikulu ya Marekani ni sehemu rasmi iliyotengwa kwa ajili ya ofisi na makazi ya rais wa nchi hiyo. Ikulu hii imejengwa mwaka 1800 ambapo zaidi ya marais 44 wameishi hadi sasa.
2: Ikulu ya Tajikistan
Ni nchi inayopakana na China ambayo inakadiriwa kuaw na watu Million 8. Ikulu ya nchi hii imetajwa katika list hii ikimata nafasi ya pili.
3: Astana, Kazakhstan
Kazakhstan imetajwa kama nchi yanye jengo zuri la Ikulu ikishika nafasi ya tatu katika list hii. Ikulu hiyo ilijengwa rasmi mwaka 2004.
4: Abu Dhabi, UAE
Ujenzi wa Ikulu hii uligharimu zaidi ya Dollar 490 million ambapo kwa mujibu wa ripoti mbalimbali majengo ya Ikulu hii ndiyo yaliyojengwa kwa gharama kubwa zaidi ukilinganisha na Ikulu zote duniani.
5: Prague, Jamhuri ya Czech
Ikulu hii inashikilia rekodi ya Guinness Book of Records kwa kuwa Ikulu kongwe zaidi duniani ambapo ilijengwa Karne ya 9. Kabla ya kuishi marais katika Ikulu hiyo waliishi wafalme na watawala. Imetajwa kuwa miongoni mwa Ikulu nzuri duniani.
6: Kremlin, Urusi
Ikuu hii ipo katika mjii mkuu wa nchi hiyo Moscow ikiwa imejengwa kati ya mwaka 1837 hadi 1849. Ni miongoni mwa Ikulu kongwe zaidi duniani ambapo majengo yake ya kipekee yanaifanya kuwa miongoni mwa Ikulu nzuri duniani.
7: Turkmenistan
Turkmenistan ni nchi iliyopo Asia ya Kati ikipakana na Afghanistan. Ikulu ya nchi hii inatajwa kwenye list ya Ikulu zenye majengo mazuri duniani. Ilijengwa mwaka 1997 na kufanyiwa ukarabati mwaka 2011. Kwa mujinu wa ripoti mbalimbali, Rais wa nchi hiyo Saparmurat Niyazov ndiye alibuni mchoro wa jengo la Ikulu hiyo.
8: Unity, Cameroon 
Ikulu ya Cameroon ilijengwa mwaka 1982 ambapo kwa mujibu wa list hii inakamata nafasi ya nane miongoni mwa nchi zenye majengo mazuri ya Ikulu duniani. Inashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na Ikulu nzuri barani Afrika.
9: Taipei, Taiwan
Ikulu ya Taiwan imeshika nafasi ya tisa kati ya Ikulu zenye majengo mazuri duniani. Ilijengwa kwa namna ya pekee baada ya kulipuliwa wakati wa Vita ya Pili ya Dunia mwaka 1945.
10: Accra, Ghana
Ghana ni miongo mwa nchi zenye Ikulu yenye majengo mazuri duniani. Majengo ya Ikulu hiyo yalijengwa mwaka 2008 yakiigharimu nchi hiyo Dollar 50 million.
Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment