Leo
asubuhi Rais John Pombe Magufuli amemteua Mshauri wa Chama chetu Prof.
Kitila Mkumbo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Chama
cha ACT Wazalendo kimepokea kwa mikono miwili taarifa juu ya uteuzi wa
mshauri wa chama chetu Kwa sababu imeonyesha kuwa Rais ameona kuwa hata
Watanzania walio kwenye Vyama vya Upinzani wana uwezo, weledi na
uzalendo wa kutumikia nchi yetu.
Kwa
nafasi hii ya Ukatibu Mkuu wa Wizara, ndugu Kitila hawezi kuendelea
kuwa Mshauri wa Chama nafasi ambayo inamfanya kuhudhuria vikao vyote vya
Chama ikiwemo Kamati Kuu.
Ndugu
Mkumbo ameandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya mshauri wa Chama na
kubaki kuwa mwanachama wa kawaida tu. Nimeipokea barua yake na
kumkubalia Kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
ACT
Wazalendo tunamshukuru ndugu Kitila Mkumbo kwa mchango wake katika
uongozi wa Chama chetu kwa wakati wote ambao alikitumikia Chama chetu
kama mshauri wa chama.
Msimamo
wa chama chetu ni utumishi wa kizalendo kwa Taifa utokanao na kila
mwananchi, ndio msingi wa kaulimbiu yetu ya ‘Taifa Kwanza, Leo na
Kesho’, hivyo basi tunamtakia kila la kheri ndugu Kitila katika utumishi
wake kwa Taifa letu katika nafasi yake hii mpya.
Wizara
Hii ni kubwa na muhimu Sana kwa nchi yetu. Maji ni tatizo moja kubwa
ambalo wananchi wetu wanakumbana nalo na Kama Taifa hatujaweza
kulimaliza.
Tunamtakia
kila la kheri ndugu Mkumbo katika kuongeza nguvu kumaliza kero ya maji
na kuhakikisha tunaimarisha Kilimo cha Umwagiliaji nchi nzima. Tunamsihi
aanze na ajenda ya Mfuko wa Maji Vijijini na kuanzishwa Kwa Wakala wa
Maji Vijijini utakaosimamia upatikanaji wa Maji Kwa wananchi wetu.
Kwa hatua hii, tunaona Rais ameamua kuunganisha nchi yetu Kwa kufanya kazi na watu wote bila kuwabagua Kwa itikadi zao za vyama.
Watanzania
ni wamoja na kauli za kuwagawa zinaumiza zaidi Taifa kuliko kuliweka
pamoja. Tunaamini kuwa Rais Ana nia njema katika uteuzi huu na sisi
tumempa baraka zote Mwanachama wetu mwanzilishi wa Chama kwenda kwenye
nafasi ya juu zaidi ya utumishi wa umma. Tunaamini hatamwangusha Rais na
muhimu zaidi hatawaangusha Watanzania.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama – ACT Wazalendo
Aprili 4, 2017
Dodoma
0 comments:
Post a Comment