Baada
ya kupiga bao mbili wakati Simba ikiitwanga Mbao FC kwa mabao 3-2,
mshambuliaji Frederic Blagnon amesema anataka kuendelea kufunga mabao
zaidi katika mechi zilizobaki.
Blagnon
alitokea benchi wakati Simba ikiwa nyuma kwa mabao 2-0, akafunga mawili
ya kusawazisha katika dakika ya 83 na 86 na kuiwezesha Simba kuibuka na
ushindi huo wa 3-2.
“Nimefurahi kutoa mchango huo kwa timu, lakini nataka kufunga zaidi katika mechi zilizobaki.
“Furaha kubwa ya mshambuliaji ni kufunga mabao, baada ya mabao hayo mawili naona nimeamka. Nataka kufunga tena,” alisema.
Simba
ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0 hadi katika dakika ya 82 lakini ikapundua
kabati kwa kusawazisha yote mawili, kabla ya kufunga la tatu.
0 comments:
Post a Comment