Jeshi la Polisi limetumia silaha za moto kuwatawanya wafanyabiashara katika eneo la Mwenge, wilayani Kinondoni leo.
Taharuki
iliwakumba wakazi wa eneo hilo mara baada ya polisi hao kuanza
kuwatanya wafanyabiashara hao waliofunga barabara wakishinikiza magari
yaruhusiwe kupaki katika eneo hilo.
Inaelezwa
kuwa polisi wamezuia watu kupaki magari katika eneo hilo hali
iliyosababisha wafanyabiashara hao kutofungua biashara zao leo.
Mmoja
wa wafanyabiashara na shuhuda wa tukio hilo, Musa Godwin alisema polisi
walifika sokoni hapo saa12 asubuhi na kutawanya wafanyabiashara
waliofunga barabara kuzuia polisi magari yasiegeshwe eneo hilo.
"Walifika
hapa sokoni saa 12 asubuhi na baadhi ya watu walifunga njia
ikasababisha polisi wapige risasi hewani, hadi sasa wanazunguka hapa
kuzuia magari ambao ni wanunuaji wetu," alisema Godwin.
0 comments:
Post a Comment