Mahakama
ya Wilaya ya Hai imemhukumu Daudi Maulid (22) mkazi wa Kijiji cha
Longoi, Kata ya Masama Rundugai, kutumikia kifungo cha miaka 30 jela na
viboko vitano baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi na
kumsababishia ujauzito.
Hukumu
hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Arnold Kirekiano baada ya
kuridhika na ushahidi wa mashahidi watano uliotolewa mahakamani.
Miongoni mwa mashahidi hao ni mwanafunzi huyo, Dawati la Jinsia na Watoto na daktari.
Hakimu alisema anatoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo katika jamii.
Alisema
kwa kosa la kubaka atatumikia kifungo cha miaka 30 jela na viboko
vitano na kosa la kumpa mimba mwanafunzi atatumikia kifungo cha miaka
mitatu na kulipa fidia ya Sh500,000.
Awali,
mwendesha Mashtaka wa Polisi, Valeria Banda alidai mshtakiwa alitenda
kosa hilo Oktoba 7, 2015 katika kijiji hicho huku akijua anafanya kosa.
Mshtakiwa
alidaiwa kumbaka mwanafunzi huyo aliyekuwa na miaka 16 ambaye alikuwa
anasoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Patmos iliyopo
wilayani hapa na kumpatia ujauzito.
Kabla ya hukumu kutolewa, upande wa mashtaka uliiomba Mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya mshitakiwa.
0 comments:
Post a Comment