Maafa ya mvua Mkoani Katavi Watu sita wafariki dunia, 47 wajeruhiwa Posted on April 2, 2017

mafuriko-mpwapwa 

WATU sita wamefariki dunia katika kijiji cha Latibili kata ya Kasansa na Igalukilo kata ya Kilida vilivyopo kwenye Halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoani Katavi na wengine 47 kujeruhiwa kutokana na mvua kubwa iliyonyeha kwa zaidi ya saa 12 ambayo pia imesabaisha kaya zaidi ya ishirini kukosa makazi.

Mkuu wa wilaya ya Mlele Bi Rachel Kasanda ametoa agizo la kufungwa shule ya msingi Kilida na wanafunzi wake kuhamishiwa kwenye shule nyingine ili waweze kuendelea na masomo kutokana na shule hiyo kujengwa katika mkondo wa maji, ambapo vyumba viwili vimebomolewa na mvua hiyo.

Mkuu huyo wa wiliya akiwa na kamati ya ulinzi na usalama alifika kijijini hapo kujionea maafa hayo na kushiriki kuwapa pole wafiwa waliokumbwa na msiba ambapo mganga mkuu wa Halmashuri ya Mpimbwe anaeleza namna alivyowapokea majeruhi na kuthibitisha idadi ya vifo vilivyotokea.

Watu 6 Wafariki Dunia Mkoani Katavi 

 

Watu 6 na wengine 47 wamefariki dunia wilayani Mlele mkoni Katavi baada ya mvua kubwa kunyesha zaidi ya masaa kumi na mbili.

 








Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment