Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA limezindua
zoezi la ugawaji vitambulisho kwa watumishi wa umma mkoani Rukwa.
Uzinduzi huo umefanywa na mkuu wa mkoa wa Rukwa Zelothe stevin katika hafla iliyo
fanyika ofisini kwake na kuhudhuliwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo
ambapo baadhi yake wamekabidhiwa vitambulisho vyao.
Aidha mkuu wa mkoa wa Rukwa ameiagiza nida kuwaandaa
wananchi kwa kutoa elimu kabla ya kuanza kuwasajili ili waweze kutayalisha
viambata muhimu vinavohitajika kuonesha wakati wa kujiandikisha kwaajili ya
kupatiwa vitambulisho.
Afisa wa Nida mkoani Rukwa EMANUEL MJUMI amesema usajili na utambuzi utaanza hivi punde kwa
wananchi waliotimizi umri wa miaka 18 na kuendelea na baadhi ya wadau wameeleza
namna walivyo lipokea zoezi hili.
Mimi nilikuwa nimesafiri sikupa taarifa ya vitambulisho vya taifa, nifanyeje
ReplyDeleteMimi nilikuwa nimesafiri sikupa taarifa ya vitambulisho vya taifa, nifanyeje
ReplyDelete