Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, ameahidi Roma Mkatoliki, Moni
pamoja na wengine wawili watapatikana Jumapili hii baada ya wasanii hao
kutekwa na watu wasiojulikana Jumatano hii wakiwa Tongwe Record.
Alisema
hayo jana akiwa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam, muda
mchache baada ya kutembelewa na wasanii ambao walimtaka mkuu huyo
kuwasaidia kupatikana kwa wasanii hao.
Akiongea
na waandishi mbele ya wasanii hao, RC Makonda alisema kila mtanzania
ana nafasi ya kumtafuta Roma na wenzake kwa kuwa hakuna anayejua watu
hao wako wapi.
“Natoa
pole kwa ndugu pamoja na marafiki, hakuna mtu ambaye anaweza kupotelewa
na mtu akawa na furaha na bahati mbaya tunahangaika kujua wapi waliko.
Nitumie fursa hii kuwaambia wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kwamba
tunapopotelewa na ndugu zetu katika mazingira ambayo hatuyafahamu sio
wakati ya kuyarusha rusha maneno na kufika hatua tunapoteza ushahidi,” alisema RC Makonda.
Alisema
tayari ameliagiza jeshi la polisi kufuatia suala hilo kwa ukaribu zaidi
ili kupata ufumbuzi mapema huku akiahidi mpaka Jumapili hii watu wao
watakuwa wamepatikana.
==>Msikilize hapo chini akiongea
0 comments:
Post a Comment