NAMNA BAO LA MUZAMIRU DHIDI YA MBAO LILIVYOFANYA AVEVA APOTEZE FAHAMU

 

Furaha ilisababisha Rais wa Simba, Evans Aveva kupoteza fahamu.

Hii ilitokea baada ya Simba kupata bao la tatu katika dakika za nyongeza dhidi ya Mbao FC na kuifanya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Simba imeibuka na ushindi huo baada ya Muzamiru Yassini kufunga bao la tatu.

Hadi Mapumziko Mbao FC ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


Taarifa zinaeleza, Aveva hakutarajia bao hilo na wakati anainuka kushangilia, alipoteza fahamu.

Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment