Mbunge
wa Kilombero kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe.
Peter Lijualikali jana amefanikiwa kuachiwa huru na maafisa wa gereza la
Ukonga baada ya kukamilisha taratibu za kutoka gerezani.
Akizungumza
mara baada ya kutoka gerezani Mbunge Lijualikali aliwataka watanzania
kutumia demokrasia ya kweli katika kutafuta majawabu ya matatizo
waliyonayo ili kubadili taswira ya Tanzania na kuwa nchi ya maendeleo
na kuongeza mshikamano bila kubaguana.
Kwa
upande wake baba mzazi wa Mbunge huyo Amberose Lijualikali aliviomba
vyombo vya dola nchini kufuata sheria za nchi zinavyoelekeza katika
kutoa maamuzi.
Kwa
upande wake Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani
Mhe. Fredrick Sumaye aliyekuwepo katika gereza la Ukonga Dar es Salaam
wakati mbunge huyo akiachiwa, aliwataka viongozi na watanzania kutumia
demokrasia katika kudai haki zao ili kulinda amani ya nchi iliyopo.
Hukumu
ya Lijualikali ilitenguliwa jana na Mahakama Kuu baada ya kukaa
gerezani kwa zaidi ya siku 70 akituhumiwa kufanya vurugu katika uchaguzi
wa mwaka 2015. Katika hukumu hiyo, Lijualikali alihukumiwa bila kupewa
masharti ya faini.
0 comments:
Post a Comment