Kiungo Mzambia,
Justine Zulu alilazimika kutoka nje dakika ya 30 na nafasi yake
kuchukuliwa na Emmanuel Martin baada ya kukumbana na kiatu cha nahodha
wa Azam FC, Himid Mao.
Yanga imeitwanga Azam FC kwa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Awali ilionekana kama
mzaha, lakini Zulu ameshonwa zaidi ya nyuzi tatu na imeelezwa huenda
itachukua kuanzia wiki mbili hadi mwezi kwake kurejea tena uwanjani.
Hata hivyo, mmoja wa wauguzi waliomchukua kumtoa nje, amesema inawezekana akapona haraka.
Zulu alipiga shuti na Himid akaingiza mguu, iinaonekana kiatu ndiyo kilichomjeruhi.
Himid Mao amuomba msamaha Justine Zulu
0 comments:
Post a Comment