Wafanyabiashara
wa nyama ya ng’ombe wilayani sumbawanga mkoani Rukwa wagoma kufanya biashara hiyo kuanzia leo
april 18.
Wakizungumza
na chemchemi radio wakiwa katika machinjio hayo ya nyama yaliyopo maeneo ya
malangali mjini sumbawanga wafanyabiashara hao wamesema hawata fanya biashara
hiyo mpaka pale serikali itakapo wasikiliza na kutatua kero zao.
Wamesema changamoto
kubwa wanayo kabiliana nayo ni kutokana na kutokuwa na miundombinu iliyo bora
katika minada ya ng’ombe inayoweza kuwafanya wao kusafirisha mifugo yao kwa njia ya usafili
kitendo kinachowafanya kusafirisha mifugo hiyo kwa njia ya kuswaga mpaka
machinjioni.
Hali hiyo
imewafanya wafanyabiashara hao kuanzisha mgomo na kusema kuanzia leo hakuta
kuwa na huduma ya nyama ya ng’ombe katika machinjio hayo mpaka pale serikali
itakapo kaa na kuwasikiliza wafanyabiashara hao.
na mwandishi wetu peter kapol'a kutoka Rukwa
0 comments:
Post a Comment