Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Kitila Mkumbo amemshukuru Rais
Magufuli kwa kumteua kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo akichukua nafasi ya Mhandisi Mbogo
Futakamba ambaye amestaafu.
Prof.
Mkumbo ambaye pia ni kada na mshauri wa Chama cha ACT Wazalendo
kinachoongozwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amesema Rais
amempa heshima kubwa kwa nafasi hiyo, na yeye kama mtumishi wa umma
hawezi kuikataa kwa kuwa ni kazi aliyotumwa na mkuu wa nchi.
"Ukishapewa
kazi na mkuu wa nchi, unaipokea na unaifanya kwa bidii kama yalivyo
matarajio, kwahiyo nimepokea uteuzi, nimekubali, mkuu wa nchi akikupa
kazi utaikataa vipi, mkuu wa nchi akikupa kazi unaifanya, kumbuka mimi
ni mtumishi wa umma" Amesema Prof Kitila
0 comments:
Post a Comment