Mbunge
wa Chemba Juma Nkamia leo alipata nafasi ya kusimama Bungeni Dodoma
katika kuchangia maoni kuhusu mapitio ya mapato na matumizi ya fedha za
ofisi ya Waziri mkuu na ofisi ya bunge kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Katika
vitu alivyoongelea Nkamia ni kitendo cha Waziri wa Habari, utamaduni,
sanaa na michezo Dr. Harrison Mwakyembe kwenda katika mkutano wa msanii
Roma mkatoliki alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es
salaam jana.
Amesema: Jana
nilipata nafasi ya kuangalia Press Conference ya Roma. Najiuliza,
Waziri wa habari alienda kufanya nini? Akiambiwa ndo alimteka Roma
atakataa?
"Mtu
alitekwa, serikali ndo inamwandalia press conference na kuisimamia? Ivi
kesho mkiambiwa ndo mlihusika kumteka mtakataa? Najua ukweli unauma,
lakini lazima tuseme.
"Serikali wakati mwingine mnaingia kwenye mitego wenyewe na mnamgombanisha Rais na wananchi.
"Nimesema ukweli, wengine wataanza kuwaza labda ni kwa sababu nilikosa uwaziri.....No, lazima tuseme ukweli."
0 comments:
Post a Comment