Mamlaka
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza mabadiliko
ya bei za mafuta nchini zitakazoanza kutumika kuanzia kesho, huku mafuta
ya petroli yakionekana kushuka.
Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli, dizeli na ya taa zimebadilika ikilinganishwa na beo za Machi Mosi mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa Habari leo katika Makao Makuu ya ofisi za EWURA, Meneja
Mawasiliano ma Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo amesema, bei ya reja reja
ya petroli imepungua kwa Shilingi tatu kwa lita ambayo ni sawa na
asilimia 0.13, pianbei ya jumla imepungua kwa Shilingi 5.65 kwa lita
sawa na asilimia 0.29.
Aidha
Kaguo amesema bei ya rejareja ya Dizeli imepanda kwa Shilingi saba kwa
lita sawa na asilimia 0.36 wakati bei ya jumla ikiwa imepanda kwa
Shilingi 3.68 kwa lita sawa asilimia 0.21.
"Hii
shilingi tatu inaweza kuonekana ni ndogo lakini ina impact () kubwa
sana kwa jamii, kwa kiasi kikubwa mabadiliko haya yametokana na
mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia, mfumuko wa bei, pia
gharama za usafirishaji ikilinganishwa na mwezi uliopita," amesema
Kaguo.
==>Bei zota ziko hapo chini.....Tazama jedwali hili
0 comments:
Post a Comment