Baada
ya kupokelewa kwa shangwe katika ukumbi wa bunge leo hii, Rais wa awamu
ya nne, Jakaya Kikwete amesema ni zamu yake kwa sasa kumuunga mkono
mkewe Mama Salma Kikwete.
Kikwete
aliyekuwa ameambatana na familia yake, ameshuhudia mkewe akila kiapo
cha ubunge katika kikao cha kwanza cha bunge lililoanza leo mjini
Dodoma.
Salma
Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa WAMA, alionekana kuwa mstari wa mbele
kumuunga mkono mumewe wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya
kulitumikia taifa.
“Leo
asubuhi nmeshuhudia kiapo cha mke wangu, mheshimiwa Salma Rashd Kikwete
kuwa mbunge wa kuteuliwa bungeni Dodoma. Ni zamu yangu kumuunga
mkono,”alinukuliwa Kikwete katika akaunti yake ya twiter.
Kikwete aliingia ndani ya bunge hilo huku akishangiliwa na idadi kubwa ya wabunge wa bunge hilo.
0 comments:
Post a Comment