Kikosi cha Yanga kitafanya mazoezi yake ya mwisho jijini Dar es Salaam, leo jioni.
Yanga
watafanya mazoezi hayo kabla ya kuondoka kwenda Algeria kuwafuata MC
Alger ya Algeria katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho.
Katika
mechi ya kwanza, Yanga iliwavurumisha Waarabu hao kwa bao 1-0 na
italazimika kufanya kazi ya ziada kuhakikisha inalinda ushindi huo.
Mazoezi
ya mwisho ambayo yatafanyika jijini Dar es Salaam yatakuwa ya mwisho
kabla ya Yanga kuanza safari ya kwenda Algeria kesho.
Yanga
ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa baada
ya Azam FC kung’olewa na Mbabane Swallows ya Swaziland.
0 comments:
Post a Comment