Leo May 17, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli ametoa mwezi mmoja kwa taasisi binafsi na za serikali kulipa madeni wanayodaiwa na JWTZ.
Rais Magufuli amezitaka taasisi hizo kuwajibika kulipa deni hilo na kuongeza kuwa atahakikisha anasimamia mchakato huo na pesa itakayopatikana isaidie kuendelea kuwekeza kwenye viwanda.
“Wote wanaodaiwa na SUMA JKT nawapa mwezi mmoja, wawe wamelipa, baada ya mwezi mmoja, vyombo vya ulinzi na usalama, muwasake wote ambao wame ‘default’. Kukopa harusi kulipa matanga, na mimi nataka iwe kukopa harusi na kulipa iwe harusi,” amesema Rais Magufuli
“Mtu akishaanza kuchezea jeshi, anadaiwa halafu halipi, hiyo ni dharau, yaani unadharau hadi jeshi !!? – Rais Magufuli
“Niwaombe wote wanaodaiwa madeni kwa kuchukua matrekta, mimi niwape mwezi mmoja. ndani ya mwezi mmoja wawe wamelipa, baada ya mwezi mmoja vyombo vyote vya ulinzi na usalama vianze kuwasaka wote.” – Rais Magufuli
Kauli hizo amezitoa JPM kufuatia ombi la Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo ambaye alisema kupitia SUMA JKT wanazidai taasisi binafsi shilingi BILIONI 40 na taasisi za umma shilingi BILIONI 3.4 na kumuomba Rais Magufuli kuwasaidia katika ulipaji wake.
0 comments:
Post a Comment