Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, amesema mmiliki wa lori lililokutwa na mizoga ya ng’ombe 12, Tegeta jijini Dar es Salaam hivi karibuni, amekamatwa.
Pia amesema mmiliki wa machinjio ilikokutwa mizoga hiyo ametoroka na serikali inaendelea kumtafuta ili afikishwe katika vyombo vya sheria.
Mpina amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo Mei 16, alipokuwa akijibu mwongozo wa Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda (CCM), aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali dhidi ya wahusika wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa Waziri Mpina lori hilo lilikuwa na ng’ombe 54 wakiwamo wazima 42, mizoga 12 na ng’ombe wanne wakiwa wamechunwa ngozi.
Tukio la kuonekana kwa lori hilo lenye lenye ng’ombe vibudu 12, lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili Mei 13, mwaka huu baada ya dereva wa lori hilo lenye namba T486DHZ kulitelekeza maeneo ya Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam jirani na machinjio.
0 comments:
Post a Comment