Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu amewataka wananchi kuchukua tahadhari hasa usiku baada ya waendesha bodaboda watatu kuuawa katika mazingira yanayofanana kwa kuchomwa na vitu vyenye ncha kali.
Kijuu ametoa kauli hiyo leo Mei 16, 2018 wakati akijibu swali katika mkutano wake na waandishi wa habari.
Amesema hadi sasa watu waliouawa ni watatu na kwamba uchunguzi unafanyika kuhusu matukio hayo, “wahusika wote watakamatwa maana Serikali ina mkono mrefu.”
Amewataka wananchi kumpelekea taarifa ofisini kwake ikiwa watapata uoga kupeleka taarifa hizo sehemu nyingine.
Kwa mujibu wa Kijuu, waendesha pikipiki waliouawa hivi karibuni pikipiki zao zilikutwa eneo la tukio huku maeneo mbalimbali ya miili yao yakiwa yamechomwa na vitu vyenye ncha kali.
0 comments:
Post a Comment