Msanii mkongwe wa taaarabu nchini Khadija Kopa amefunguka na kuzungumzia hali ya taarabu ilivyo sasa nchini na kusema kuwa wasanii wengi wamekuwa jeuri na kwamba hawajitunzi kama zamani hivyio wanajishusha thamani wao wenyewe na wala sio kitu kingine.
Khadija kopa anasema kuwa wasanii wa taarabu wamekuwa wakiimba katika ma bar kwa kiinglio cha bia wakati hiyo haikuwa kama zamani na ili kukomesha hilo waimbaji hao wanatakiwa wakifuatwa wasikubali kufanya hivyo na kujiona wa thamani ili kupanda hadhi yao.
Hata hivyo akizungumzia swala la yeye kustaafu kama alivyofanya gwiji wa taarabu nchini, mzee Yusup, malkia huyo amesema kuwa alichokifanya mzee ni kutokana na imani yake ilivyomtuma na ni jambo zuri , hata yeye siku yoyote atastaafu na sio muda mrefu kutoka sasa kwa sababu anahitaji kutenga muda mwingi pia kwa ajili yake , dini na mungu wake kwa sababu hajuai siku wala saa ya kufa kwake.
Hata hivyo Khadija Kopa anasema kuwa kama ataamua kufanya hivyo atafanya kimya kimya bila kumwambia wala kutangaza kwa watu, bali watashangaa tu haingii tena studio wala haonekani tena katika maswala ya burudani.
"Sina muda mrefu sana nitaacha huu muziki na nitakapo acha wala sina haja ya kutangaza eti eeh ninaacha muziki, hapana nitaacha tu na watu wataona kimya tu sitoi nyimbo.
0 comments:
Post a Comment