VIDEO: “Nilikamatwa kama mnyama” – Nay wa Mitego

 

April 4, 2017 kupitia XXL ya Clouds FM msanii wa Bongo Fleva Nay wa Mitego alizungumzia kuhusu tukio lake la kukamatwa kisha kuachiwa na polisi na baadaye kumtembelea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dr. Mwakyembe mjini Dodoma.

Rapa Nay wa Mitego amedai hakukuwa na jambo lolote baya lililomtokea wakati anakamatwa akisema kuwa amewasamehe waliomkamata ingawa alikamatwa kama mnyama….>>>“Hakuna kibaya. 

Vimetokea na tayari vimepita, nilikamatwa kama mnyama na nimewasamehe walionikamata. Nilikuwa nimemaliza show Turiani, nikiwa hotelini Polisi walikuja kunifuata. Nikauliza kuna nini? Sikujibiwa chochote na nilipelekwa mpaka kama vituo vitatu vya Polisi baadaye nikapelekwa Dar es salaam lakini kosa sikufahamu.

” – Nay wa Mitego.
>>>”Nimshukuru sana Rais Magufuli kwa kuwa muelewa na kutambua Uhuru wa mawazo ya kazi ya Sanaa na wimbo huu ulitoka kwa ajili ya maudhui ya maisha yaliyopo kwa sasa sababu kazi ya Sanaa inahitaji ubunifu. 

Siyo wote wanapenda huu wimbo wa WAPO uendele kuwepo ila Wapo wanaotaka kuufuta huu wimbo usisikike kabisa.” – Nay wa Mitego.
Bonyeza Play hapa chini kusikiliza full interview

 

VIDEO: ‘Natamani siku moja nirudi shule kusoma’- Dogo Janja

 



Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment