Mbunge
wa Jimbo la Mtama mkoani Mtwara kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Nape Nnauye
amtaka Rais Magufuli aunde tume huru ambayo itaweza kuchunguza matukio
ya uhalifu ya uvamizi wa studio unaoendelea nchini.
Hatua
hiyo inatokana na matukio ya kiuhalifu yanayoendelea Tanzania na kuacha
maswali mengi vichwani mwa wananchi kushindwa kufahamu kuwa watu hao na
vikundi hivyo vya kihuni vinavyofanya vitendo hivyo vinapata wapi
mamlaka hayo kuwa na nguvu kushinda Dola.
“Ombi
langu kwa Rais namuomba aunde tume huru ichunguze matendo haya
yasijirudie tena kwa sababu yasipochukuliwa hatua yataharibu sura ya
Tanzania pia yataweza kuibuka makundi ya wahuni kuanza kuteka watu nao
kwa kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa. Tumsaidie Rais Magufuli kwa
kumwambia ukweli naimani atasikia na atafanyia kazi kwa kuwa Rais wetu
anapenda kusikiliza watu”. Alisema Nape
Aidha
Mbunge huyo amesema watu wanaofanya mambo hayo wanalengo la
kuwagombanisha wananchi na Rais wao jambo ambalo sio zuri kwa taifa.
"Juzi
amepotea msanii Roma Mkatoliki na wengine lakini mpaka sasa haifahamiki
wapo wapi, yaani kama vile amepotea Nzi, tulisikia kijana mmoja wa
CHADEMA anaitwa Ben Sanane amepotea saizi miezi mitano imepita, matendo
haya ya kina Ben Sanane, Roma Mkatoliki, na wengine yanajenga chuki ya
wananchi kwa Rais, lakini pia yanajenga chuki kwa wananchi na Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ". Alisema Nape Nnauye
0 comments:
Post a Comment