Mahakama ya Kazi nchini Kenya imeweka zuio la muda dhidi ya serikali ya nchi hiyo kuajiri madaktari kutoka nje ya nchi hiyo.
Jaji
Nelson Abuodha wa Mahakama hiyo ametoa amri hiyo baada ya Madaktari
watano wa Kenya kufungua malalamiko ya kuitaka serikali kusitisha mpango
wake wa kuajiri madaktari 500 kutoka Tanzania wakidai kuna madaktari
wengi nchini humo ambao hawajaajiriwa.
Madaktari
hao wameitaka Mahakama itoe amri inayoitaka serikali kuajiri madaktari
1,400 ambao hawana ajira ambao wamefuzu katika taaluma ya utabibu na
iizuie serikali kuacha kabisa kuajiri madaktari na wataalam wengine wa
afya kutoka nje.
Hatua
hiyo imekuja baada ya Rais Magufuli kukubali ombi lilitolewa na Rais
Uhuru wa kuipatia Kenya madaktari katika kusaidia utoaji tiba baada ya
kutokea kwa mgomo wa madaktari nchini humo wenye lengo la kushindikiza
waboreshwe maslahi yao.
0 comments:
Post a Comment