VIDEO: Mbunge Lijualikali alivyopokelewa na wananchi wa Jimbo lake Kilombero By Makoleko TZA on April 8, 2017

 

Wananchi wa Jimbo la Kilombero mkoani Morogoro, wamempokea kwa furaha na shangwe kubwa Mbunge wa Jimbo hilo Peter Lijualikali ‘CHADEMA’ wakati anawasili jimboni mwake baada ya kutoka gerezani.
March 30, 2017 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilitengua hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya Kilombero dhidi ya Mbunge Peter Lijualikali baada ya kukiri kuwa hati ya mashtaka iliyomtia hatiani Mbunge huyo ilikuwa na mapungufu.
Mbunge Lijualikali aliwasili Jimboni humo akisindikizwa na Wabunge wengine wanne ambao ni Joseph Haule, John Heche, Susan Kiwanga na Devotha Minja.
Bonyeza play hapa chini kuitazama…

 

VIDEO: Wakili kaeleza sababu za Mbunge Lijualikali kuachiwa huru. Bonyeza play kutazama.





Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment