Unaweza
kumekucha kwa kuwa Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga imeitaka Bodi
ya Ligi Kuu Bara kutothubutu kuwapa pointi tatu za mezani watani wao wa
jadi Simba.
Kamati
hiyo imekutana jana ikiwa siku chache tangu uongozi wa Simba kumkatia
rufaa beki wa Kagera Sugar Mohammed Fakhi ambaye imeelezwa alikuwa na
kadi tatu za njano kabla ya mchezo wao uliopigwa kwenye Uwanja wa
Kaitaba mjini Bukoba.
Mjumbe
wa Kamati Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi ameiambia SALEHJEMBE kuwa
wameliingilia suala hilo lililopo chini ya Kamati ya Masaa 72 ya TFF kwa
kuhofia kuwaathiri mbele ya safari wakati wakitetea taji hilo la
ubingwa.
Mkemi
alisema, tayari wamepeleka malalamiko kwa Mamlaka ya kuzuia na
kupambana na rushwa (TAKUKURU), Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na watu wa
Cyber ili kuchunguza barua pepe zilizotumwa na mwamuzi wa mchezo huo
kwenda kwa Kamati.
"Kamati
hii imechelea kutoa maamuzi kwa kuandaa ripoti za uongo za michezo
dhidi ya Fakhi pia tuna taarifa za kughushiwa email na nyaraka zingine
ili kuipa alama tatu Simba SC yenye zaidi ya wajumbe 6 katika kamati
hiyo.
"Kama
Yanga tumeanza uchunguzi wetu na kutoa taarifa kwa vyombo husika vya
dola pia maamuzi yoyote ya kuibeba Simba tutakwenda mahakamani licha ya
sheria za FIFA kukataza hivyo kama hawataki tufike huko lazima haki
itendeke.
"Tumeshavijulisha
vyombo husika yaani Takukuru, watu wa (cyber crime) na TCRA juu ya
uchunguzi wa mawasilano ya waamuzi wote waliosika na kutajwa kwenye
rufaa hiyo" alisema Mkemi.
mwisho
0 comments:
Post a Comment