KATIBU
mtendaji wa haki za binadamu kanda ya Sumbawanga mwinjilisti
Silivesta lupamba ameingia kwenye wakati mgumu baada ya
kufukuzwa kijijini kwake na uongozi wa kijiji cha ilimba
kata ya Mkoe wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa kwa madai ya
kula fedha za kijiji kiasi cha shilingi milioni moja{1000000/=} pamoja na kuendekeza maswala ya kisiasa miungoni mwa wananchi.
Akiongea na kituo hiki mara baada ya kufukuzwa kwake
kijijini hapo kiongozi huyo wa haki za bidamu kupitia kwenye
kikao maalumu kilicho shirikisha wanasheria na viongozi wa haki
za binadamu kutoka mikoa ya Rukwa na katavi na kushirikisha
wananchi wa kijiji hicho.
Amesema uongozi wa kijiji hicho
umemwandikia barua ya kutakiwa kufungasha kila kilicho chake na
kuondoka kijijini mara moja kwa madai ya kula fedha za kijiji
kiasi cha shilling milioni moja {1000000=} kitu ambacho si
kweli.
Amesema
anashangazwa na kitendo cha uongozi wa kijiji hicho
kumwandikia barua ya kutakiwa kuondoka kijijini kwake na
wakati yete ni mtanzani halisia.
Mkurugenzi
wa mashirika ya haki za binadamu kanda ya Sumbawanga na
katavi Dr . John Masiah , amesema wanalani kitendo cha
kufukuzwa kwa kiongozi mwenzao kutokana na kwamba ni kinyume na
sheria za nchi.
Wananchi wa kijiji hicho kwa upande wao walikuwa na maoni tofauti kuhusikana na sakata hilo.
0 comments:
Post a Comment