Mahakama
ya Wilaya ya Mbeya, imemuhukumu kifungo cha nje cha miezi sita na
kulipa faini ya Sh1 milioni, Aman Mwasote baada ya kutiwa hatiani kwa
kumwita mtoto wa miaka tisa kuwa mchawi.
Mwasote,
ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili alishtakiwa kwa kutoa kauli kuwa
mtoto huyo huwaloga wanafunzi na walimu alipokuwa kwenye mkutano wa
injili.
Hukumu
hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi, Venance Mlingi aliyesema mahakama
imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne wa upande wa
Jamhuri kwamba, Mwasote alitenda kosa hilo.
Awali,
Wakili wa Serikali, Xaveria Makombe alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo
Septemba 20, mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Kalobe, akiwa kwenye
mkutano wa hadhara wa Injili.
Hakimu
Mlingi alisema mshtakiwa atatumikia kifungo cha nje kwa kufanya
shughuli za kijamii na Aprili 20 atatakiwa kufika mahakamani ili
apangiwe shughuli ya kufanya.
0 comments:
Post a Comment