VIONGOZI serikali
za vitongoji na vijiji pamoja
wajumbe katika kata ya Mnamba
wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wamesusia kikao
cha mh. diwani wa kata hiyo Maiko Jimsoni
Chilulumo wakitaka kupewa chakula
kabla ya kuingia kwenye kikao sambamba
na kulipwa posho.
Hali hiyo ya
kushangaza imejitokeza wakati wa
kikao maalumu kilicho kuwa kimeitishwa
na diwani wa kata hiyo Maiko Jimsoni Chilulumo kilichokuwa
na lengo la kujadili shughuri
mbalimbali za maendeleo ya kata hiyo na
kufanyika katika kijiji cha Luse.
Wakiongea na kituo
hiki mara baada ya kususia kikao
hicho viongozi hao, wamesema chanzo
nikutokana na uongozi wa kata hiyo
kuto wajari kwa kuto wandalia chakula
wakati wa vikao mbalimbali ambavyo
vimekuwa vikifanyika na kuwa
watahudhuria vikao mpaka pale
watakapo wekewaa bajeti ya ya
chakula wakati wa kikao
Mtendaji wa
kata hiyo Ebeneza Laiza amesema
hali hiyo imekuwa ikipelekea kushindwa
kuendesha shughuri za maendeleo kutokana na viongozi
wa vijiji pamoja na wajumbe kugoma kuingia
kwenye vikao wakitaka chakula na posho
na kuwa hilo ni tukio la tatu
kutokea.
Diwani wa kata hiyo
Maiko Jimsoni Chilulumo amelani kitendo
hicho na kuwa yeye kazi
yake ni kusimaamia shughuri za maendelea
na sikuleta vyakula
kwenye vikao.
0 comments:
Post a Comment