WAJUE MAPRODUCER SABA WAKALI WALIOWAHI KUTOKEA KIPINDI HICHO | WACHEKI HAPA

P. FUNK MAJANI - BONGO RECORDS
Ipo wazi P.Funk Majani ni Legend katika mziki wa Tanzania,huyu jamaa ni mbaya sana katika kutengeneza beats kali, utakubaliana na mimi ukiskiliza nyimbo kama Mvua na jua ya Jay Mo,Anakuja ya Sister P, Nini mnataka ya Pig Black, Hayakuhusu ya Rah P, Kigetogeto ya Juma Nature na nyingine Chungu mzima.
P Funk amewatoa wasanii wengi kama marehemu Ngwair(R.I.P),Juma Nature,Afande Sele, Sister P, Jay Mo, Profesa Jay na wengine chungu mzima.





MASTER JAY- MJ RECORD



Mmoja kati ya maproducer wanaojua haswa kufanya mixing kali ya musiki, anauwezo mkubwa sana wa kutambua na kuona kipaji cha mtu katika mziki.Aliweza kuibua vipaji vikubwa ambavyo vilifanya vizuri katika medani ya muziki wa Tanzania kama vile Lady Jay Dee ,Mike T Mnyalu bila kusahau Kundi la Kwanza Unit Ngoma ya Msafiri alitengeneza Master Jay na wengineo.

                                                                                                                          mtanganjia.blogspot.com
MIKA MWAMBA- FM STUDIO


Huyu ni moja ya kichwa kilichowakosesha usingizi watayarishaji wake kutokana na ubunifu wake wa hali ya juu, licha ya kufanya kazi nchini kwa muda mchache sana kabla hajarudi kwao ulaya lakini aliacha historia ya ngoma zake ambazo zinasikilizwa mpaka hii leo, mfano mzuri ni ngoma ya Balozi "wengi walikwepo",  Salome ya Dully Sykes na bila kulisahau Kundi la Daz Nundaz.

HENRICO- SOUND CRAFTERS

Henrico ni mmoja ya watayarishaji wkongwe sana nchini hapa ambaye ameweza kuibua vpaji vingi haswa kwa wasanii wengi wa Temeke, Wasanii waliowahi kufanya kazi na Henrico ni kama Inspector Harun na kundi lake la Gangwe Mobb,Mabaga Fresh,Mack Malik Simba (R,I.P) ,Solo Thang na wengine wengi.

ROY WA G RECORD (R.I.P)- G RECORD


Enzi za uhai wake Roy alikuwa ni mmoja ya vichwa vikali kwenye utayarishaji wa midundo yenye ladha za upekee na utofauti mwingi, Roy aliweza kuinua vipaji kama vya kina Mr Blue,Enika -Baridi kama hii kama unaukumbuka ule mdundo utakuwa shahidi yangu.


SAID COMORIEN-METRO STUDIO


Comorien huyu alikuwa ni fundi wa vinanda, ukiwa ugonjwa wako ni vinanda basi tafuta ngoma alizotengeneza huyu mtu. Uwezo wake wa kukung'uta vinanda upo juu sana,  sikiliza wimbo wa T.I.D wa nyota yangu usikie vile vinanda alivyoviingizia.Marehem Mez B (R.I.P) pia alishafanya kazi zake nyingi na Comorien bila kumsahau Noorah.


BONY LUV-MAWINGU STUDIO

Bony Luv ni mmoja ya maproducer wa zamani ambao ni multi-talented ,anauwezo mkubwa wa kutengeneza ngoma,kufanya mixing kali na ku dj pia.Amefanya kazi na wakongwe wengi wa zamani likiwemo kundi la Kwanza Unit waliorekodi santuri ya kwanza kabisa iliyoenda kwa jina la Kwanza Unit mwaka 1993.

Hawa ni baadhi tu ya watayarishaji waliowahi kuvuma sana enzi hizo, lakini wapo wengine wengi kama Amit Mento alitengeneza ngoma nyingi kali zikiwemo vituko  uswahilini original na remix ya Suma G aliyomshirikisha Inspekta Haroun, pia ndiye  alimyemtoa pia Mez B na ngoma ya kwanza iliitwa Fikiria, alitengeneza ngoma nyingi.za TID kama, siamini,nk pia ngoma ya Ray C uko wapi na Kuna nyimbo kama mambo safi ya Marehemu Complex,Big Dog Pose BDP majobless,na kumwambia. Pia kulikuwa na watayarishaji kama Akili The Brain,  Kameta na wengineo

Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment