Watu watatu wameuawa na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab katika eneo la pwani ya Kenya.
Kwa
mujibu wa gazeti la Star, Alshabaab walivamia basi hilo la abiria
majira ya tisa na nusu alfajiri likisafiri kutoka Mombasa kwenda Kipini.
Vifo
hivyo vilitokana na wanamgambo hao kufyatulia risasi kadhaa basi hilo
lakini Jeshi la Polisi liliwahi kufika na kujibu mapigo, hali
iliyosababisha washambuliaji hao kutokomea kusikojulikana.
Julai
27, Mratibu wa Mkoa wa Pwani, Nelson Marwa alitahadharisha watu
wanaofanya safari zao kwa magari binafsi kupitia eneo la Lamu kwenda
Mombasa kutofanya hivyo bila kusindikizwa na Jeshi la Polisi.
Alisema
kuwa kwa magari ya abiria na ya watu binafsi yatakayojaribu kupita eneo
hilo bila kusindikizwa na jeshi la polisi wataadhibiwa ikiwa ni pamoja
na kunyang’anywa leseni zao, kutokana na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha
tishio la mashambulizi ya Al-Shabaab.
Kundi
la Al-Shabaab ambalo limejikita katika nchi ya Somalia limekuwa
likiendesha mashambulizi ya kushtukiza katika baadhi ya maeneo nchini
Kenya hususan maeneo ya Pwani.
Aprili
mwaka 2015, kundi hilo lilitekeleza shambulizi baya katika Chuo Kikuu
cha Garissa lililosababisha watu 148 kupoteza maisha.
0 comments:
Post a Comment