Zikiwa ni siku mbili kupita baada ya uzinduzi wa mradi Wa umeme vijijini awamu ya tatu (rea phase iii ) ulio zinduliwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt Medard Kalemani Agosti 14, 2017 Mkoani Rukwa Meneja tanesco mkoani humo amewataka wananchi kutoa ushilikiano ili kuepukana na matapeli watakao jitokeza katika zoezi hilo.
Akizungumza na kituo hiki ofisini
kwake meneja tanesco mkoani Rukwa Mhandisi Herini
mhina amewataka wananchi
kuweza kutoa ushirikiano kwa mkandarasi aliye tambulishwa kusimamia zoezi hilo ikiwa
ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa miundombinu.
Mhina amesema kuwa mradi
huo unahitaji ushilikiswaji wa wananchi kutokana na kutokuwepo kwa ulipwaji wa
fidia na hivyo kuwataka wananchi kutoa ushilikiano kwa mkandalasi ili kuweza
kukamilisha zoezi hilo.
Pamoja na hayo Mhina ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kulinda miundombinu ya serikali ikiwa ni pamoja na kuacha tabia ya kuchoma nguzo za umeme kwani kwa kufanya hivyo wanarudisha nyuma maendeleo katika jamii.
NA
PETER KAPOLA KUTOKA RUKWA
0 comments:
Post a Comment