August 21, 2017 kupitia ukurasa wa Twitter wa mwimbaji wa Bongofleva Alikiba uliandika maneno 12 ikiwa ni ujumbe kwa mtu ambaye anaonesha kumchukia kwa asilimia huku akionesha kutojali.
Alikiba aliandika>>>”I know that you hate me 100% but I give ZERO F**ks #KingKiba”
Alikiba baada ya kuandika hayo mashabaki wakaanza kuhusisha maneno hayo na remix ya FRESH wa Fid Q ambapo Diamond ameshirikishwa na katika sehemu aliyoimba kuna maneno yanayoashiria kama kijembe kwa Alikiba.
>>>”Ukinichukia sikosi hela hivyo kwangu siyo kesi, kunikompea na Sinderela haiwezi kuwa fresh. Simba toka Mbuga ya Tandale naona Swala wana force tuwe salesale, viuno vidogo wanataka pensi ya pepekale si walitaka kiti nimewapa hadi kitanda wakalale.”
0 comments:
Post a Comment