Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemarry Sitaki akizungumza katika mkutano na wananchi katika kata ya Mabilioni wilayani Same.
Baadhi
ya wananchi katika kata ya Mabilioni wilayani Same wakimsikiliza mkuu
wa wilaya alipozunumza nao katika mkutano uliofanyika katika ofisi ya
kata.
Afisa
Elimu wa Kata ya Mabilioni wilayani Same,Richard Sekibojo akimkabidhi
taarifa ya kata hiyo Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemarry Sitaki wakati wa
mkutano uliofanyika katika ofisi za kata hiyo.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Mabilioni waliohudhuria mkutano huo.
Mkuu
wa wilaya ya Same ,Rosemarry Sitaki akifuatilia maelezo ya kero
mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na wananchi katika mkutano huo.kushoto
kwake ni Diwani wa kata ya Mabilioni,
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini..
WANANCHI
katika Kata ya Mabilioni wilayani Same wako katika hatari ya kupata
ugonjwa wa kipindupindu kutokana na kutumia maji ya mto Ruvu yaliyopimwa
na kugundulika kuwa na chembe chembe za Kinyesi cha Binadamu.
Wakazi
5109 wanaounda kaya 1158 wamekuwa wakitumia maji ya Mto Ruvu unaopita
katika vijiji vitatu viliyoko kaika kaa hiyo vya Chekereni,Mabilioni na
Ruvu Mbuyuni kwa ajili ya Kunywa,Kupikia ,Kufulia ,kuogea pamoja na Kilimo .
Afisa
Elimu wa kata ya Mabilioni ,Richard Sekibojo aliyasema hayo wakati
akitoa taarifa ya kata hiyo kwa Mkuu wa wilaya ya Same, Rosemarry Sitaki
alipofanya ziara katika kata hiyo na kufanya mkutano na wananchi wa
kata ya Mabilioni.
“Mh
Mkuu wa wilaya kata ya Mabilioni haina maji safi ya kunywa,kwani
wananchi wanatumia maji ya Mto Ruvu kwa matumizi yote ya nyumbani pamoja
na Kilimo na
maji hayo yalipimwa yakaonekana kuwa yana chembechembe za kinyesi cha
binadamu zinazosababiha ugonjwa wa kipindupindu”alisema Sekibojo.
Akijibu
malalamiko hayo Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemarry Sitaki alisema uko
mradi mkubwa sana wa maji wa serikali toka wizara ya Maji ,ambao unatoa
maji Bwawa la Nyumba ya Mungu kupitia wilaya ya Mwanga,Same hadi Korogwe mkoani Tanga .
“Kuhusu
suala la maji ,nilikuwa naambiwa hapa kuwa kila visima vikichimbwa maji
yanakuwa na chumvi nyingi sana na kwamba hayawezi kutumika kama maji ya
kunywa na yale ya mtoni ndio kama tulivyosikia kuwa hayana sifa za
kiafya na kutumika na binadamu.”alisema Sitaki.
Mradi
huu mkubwa ndio utakuwa suluhu ya haya matatizo ,mradi tayari umeanza
kujengwa kwenye chanzo ukiwa katika hatua za mwisho kukamilika na katika
wilaya ya Same mkandarasi amekwisha patikana na ameanza kuchimba
matenki .
Alisema
kulingana na ukubwa wake,mradi huo utachukua hadi miaka mitatu
kukamilika kwake na kwamba utagharimu zaidi ya Sh. Bilioni 142
ukifadhiliwa na serikali kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa na
mashirika ya misaada ya kimataifa kutoka nchi za Falme za Kiarabu.
Kwa
mujibu wa serikali mkoa wa Kilimanjaro,mradi huo utawaepusha idadi
kubwa ya wananchi kwenye Wilaya hizo kuondokana na hatarini kuugua
magonjwa ya mlipuko kama Kipindupindu na Kuhara kutokana na kunywa maji
yasiyo safi na salama.
Hadi
kukamilika kwake mradi huo utanufaisha zaidi ya wananchi 247,500 wa
vijiji 28 vya Wilaya za Mwanga na Same kwa upande wa mkoa wa Kilimanjaro
ambao kwa sasa upatikanaji wa maji vijijini ni asilimia 79 na mijini
mkoa wa Kilimanjaro unakimbilia asilimia 98.
Mradi
huo unajengwa kwa ufadhili wa Benki ya Kiarabu inayosimamia Maendeleo
ya Nchi za Afrika (Badea), Mfuko wa Ofd unaojumuisha nchi zinazozalisha
mafuta (Opec) na Mfuko wa Maendeleo wa Kimataifa wa Saud na Mfuko wa
Misaada wa Kuwait.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment