Baraza
la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema kuwa linasikitishwa na hali
mbaya ya kisiasa nchini Burundi zikiwemo taarifa za ongezeko la idadi ya
wakimbizi na taarifa za mateso, kupotea kwa watu na mauaji ya kinyama.
Katika
ripoti hiyo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limesema kuwa
limekusudia kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika na matukio hayo
ndani na nje ya nchi hiyo kwakuwa wanatishia amani na usalama wa
Burundi.
Taarifa
hiyo iliyosomwa na Balozi, Amr Abdellatif Aboulatta wa Misri ambaye
ndio mwenyekiti wa Baraza hilo, amesema kuwa baraza hilo linasikitishwa
na hali mbaya ya kibinadamu inayoendelea Burundi ambapo zaidi ya
wakimbizi laki mbili wamekuwa wa ndani, huku watu raia milioni tatu
wakiwa na mahitaji na zaidi ya raia laki nne wakitafuta ukimbizi katika
nchi za jirani.
Aidha,
Baraza hilo limeshukuru nchi zinazopokea wakimbizi kwa jitihada zao,
mataifa ya kikanda kwa kuheshimu wajibu wao wa kimataifa hasa katika
kujali hadhi za wakimbizi na kuhakikisha wanarejea waliokotoka kwa hiari
yao kwa kuzingatia uamuzi wao na taarifa za usalama na utu wa binadamu.
Hata
hivyo, Baraza hilo limelaani vikali matamko ambayo yamekuwa
yakihamasisha vurugu na chuki dhidi ya raia ikiwemo wito wa kulazimisha
kuwapa ujauzito wanawake na wasichana na kuitaka Serikali na pande zote
kusitisha mara moja vurugu na kulaani kauli zote za chuki.
0 comments:
Post a Comment