Fisi akila nyama,siyo ya mwili wa mtoto katika habari
Diwani wa kata ya Lagana Boniface
Butondo (mwenye shati la Kitenge) na wananchi wakiwa karibu na kaburi la
mtoto aliyefariki kwa kuliwa na fisi)
****
Mtoto aliyejulikana kwa jina la Katambi
Masunga mwenye umri wa miaka mitano amefariki dunia baada ya kuliwa na
fisi katika Kitongoji cha Mwabuli kijiji Mwamadulu kata ya Lagana
wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea
usiku wa Agosti 8,2017 kuamkia Agosti 9,2017 baada ya fisi kuvamia
katika familia aliyokuwa anaishi motto huyo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,mtoto huyo mwenye ulemavu wa
viungo akiwa na mtoto mwenzake wakicheza nyumbani kwao majira ya saa
moja na nusu usiku siku hiyo,ghafla alitokea mnyama aina ya fisi.
“Baada ya kutokea fisi huyo watoto walianza kupiga kelele,huku mtoto
mmoja akifanikiwa kukimbia,lakini mtoto huyo mwenye ulemavu wa viungo
hakuweza kukimbia ndipo akanyakuliwa na fisi huyo”,mashuhuda wameiambia
Malunde1 blog.
Baada ya fisi huyo kumnyakua mtoto huyo,alikimbia naye
vichakani,kutokana na mayowe ya watoto, ndipo ndugu pamoja na majirani
walipoanza kumtafuta fisi huyo.
Akizungumza na Malunde1 blog,Diwani wa kata ya Lagana,Boniphace Butondo
ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu alisema
baada ya takribani dakika 30 ndipo wananchi wakafanikiwa kumpata fisi
huyo ambaye tayari alikuwa amekula miguu na tumbo la mtoto huyo.
“Baada ya wananchi kufika katika kichaka fisi akaruka na kuanza
kukimbia,waliposogea ndipo wakakuta kipande cha mwili wa mtoto
kilichobakia na kukibeba”,alisema Butondo.
“Kwa kweli hili tukio limetuhuzunisha sana,kumekuwepo na fisi wa ajabu
sana eneo hili,fisi wamezaliana sana hali inayotishia amani na kuleta
hofu kwa wananchi,tatizo la njaa pia linachangia hata wanyama wamekosa
chakula,wamekuwa wakila hata mazao”,aliongeza Butondo.
“Julai 28,2017 katika kikao cha baraza la madiwani moja ya ajenda
ilikuwa ni kuhusu tishio la fisi katika kata tano za
Itilima,Lagana,Ngofila,Uchunga na Mwamashele,tuliomba halmashauri iandae
fedha maalum kwa ajili ya kuangamiza fisi hawa,utekelezaji wa
kuwaangamiza fisi utaanza hivi karibuni”,alieleza Butondo.
Kata ya Lagana imekuwa ikikumbwa na matukio ya wananchi kuvamiwa na fisi
ambapo hivi karibuni mzee mmoja alinusurika kufa baada ya kushambuliwa
na fisi akiokoa mbuzi wake huku kukirporiwa tukio la mwanafunzi wa
darasa la nne kufariki kwa kuliwa na fisi.
0 comments:
Post a Comment