Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri, utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu.
Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini ya kiwango,
hii hupelekea watu hawa kutumia ving´arisha ngozi kama krimu, vidonge au nyenzo zingine kubadilisha ngozi zao.
Tafiti
zinaonyesha kwamba wavulana na wasichana hupendelea kutumia bidhaa
zinazong´arisha ngozi ili waweze kupata hadhi nzuri katika kundi la
familia zao, na jamii. Kwa kweli,hata matangazo yanayoonyeshwa kwenye
televisheni mbalimbali huonyesha kitu hiki.
Mambo
hayo yote huwa na athari kubwa juu ya mawazo ya vijana wa kiume na
wakike ambayo hupelekea kuwafanya wachague chochote wanachomudu kati ya
krimu au vidonge.
Madhara ya kujichubua ni yapi?
Mtu
anaeyejichubua anaweza kupata kansa ya ngozi, chunusi, uvimbe katika
ngozi, ngozi kuwa nyembamba,Kuongezeka kwa hamu ya kula na uzito,kutokwa
na mabaka, pumu, kupata watoto wenye kasoro, kupata matatizo ya akili,
kuharibika kwa ini, kuharibika kwa mishipa ya fahamu pamoja na figo
kutokana na kiwango kikubwa cha zebaki(mercury) kilichomo katika
krimu,Osteoporosis(kupungua kwa uzito wa mifupa ambapo huongeza hatari
ya kuvunjika kwa mifupa)
Baadhi ya madhara haya huonekaa mara moja na mengine hujitokeza kadri mtu anavyotumia ving´arisha ngozi.
0 comments:
Post a Comment