Jumamosi ya July 29 robo fainali ya tatu ya michuano ya Ndondo Cup 2017 ilichezwa katika uwanja wa Kinesi Dar es Salaam kwa kuzikutanisha timu za Misosi FC ya Tandalena Mpakani Kombaini ya Mabibo.
Katika mchezo huo uliyohudhuriwa na mashabiki na viongozi mbalimbali ulimalizika kwa Misosi FC kuibuka na ushindi wa magoli 3-0, mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Nnauyealikuwa miongoni mwa watu waliyohudhuria michuano hiyo na kutaja vitu vilivyomvutia katika mchezo huo.
“Ndondo kama Ndondo sasa imekuwa Brand kubwa sansa kwa sasa namna ya kushindana nayo ngumu, jambo moja kubwa ambalo nimeliona katika mechi za hapa kuna haki kubwa inatendeka, kwa upande wa mchezaji nimevutiwa na yule namba tatu wa Mpakani ningekuwa na timu ningemchukua” >>> Nape Nnauye
0 comments:
Post a Comment