Waziri wa afya ,jinsia,wazee na watoto
Ummy Mwalimu ,akitembelea kituo cha afya Mlandizi ,wa kwanza kushoto ni
mganga mfawidhi wa kituo cha afya Mlandizi,Dk.Mpola Tamambele,ambae
amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi .(Picha na Mwamvua Mwinyi )
Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini
Hamoud Jumaa ,akizungumza mara baada ya waziri wa afya ,jinsia ,wazee na
watoto Ummy Mwalimu kutembelea kituo cha afya cha Mlandizi .
****
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
WAZIRI wa afya, jinsia ,wazee na watoto
,Ummy Mwalimu ,amemsimamisha kazi mganga mfawidhi wa kituo cha afya
Mlandizi,dk.Mpola Tamambele,kutokana na kushindwa kusimamia maelekezo ya
serikali ya kuhakikisha mama mjamzito ,mtoto chini ya miaka mitano na
mzee wanapata huduma bure .
Kutokana na kutokuwa na mamlaka ya moja
kwa moja amemuagiza kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya halmashauri ya
wilaya ya Kibaha ,Beda Mmbaga kumsimamisha kazi mganga mfawidhi huyo
mara moja wakati uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili zikiendelea .
Amemuelekeza kaimu mkurugenzi huyo pia
kuwafuatilia watumishi wa afya kituoni hapo waliohusika kumuagiza mama
aliyejifungua Salma Khalifan kwenda kununua vifaa vya kujifungulia vya
sh.180,000 ili apate huduma .
Aliyasema hayo wakati alipokwenda
kutembelea kituo cha afya Mlandizi ,kabla ya kukabidhiwa kwa magari ya
wagonjwa matatu kutoka kwa mbunge wa jimbo hilo ,Hamoud Jumaa .
Waziri huyo alisema yeye hana mamlaka ya
moja kwa moja kumsimamisha kazi mganga mfawidhi huyo hivyo anaiachia
mamlaka husika isimamie jukumu hilo.
Alisema hatokubali kuona watumishi wachache kwenye vituo vya afya ,zahanati na hospitali wanachezea maagizo ya serikali.
Alifikia hatua hiyo baada ya kupokea
malalamiko kutoka kwa mama aliyejifungua ambae alisema amenunua vifaa
vya kufanyiwa operesheni kwa gharama ya sh .180,000 .
Ummy alisema haiwezekani kuona mama
wajawazito ,wanalipishwa hadi gloves na pamba ili kujifungua wakati
serikali yao ilishasema watahudumiwa bure .
Alieleza kwamba ,kuanzia sasa waganga
wakuu wa wilaya ,mikoa na watumishi wa afya wote nchini wahakikishe
wanatimiza maelekezo ya serikali kuhudumia akinamama wajawazito na
watoto ili kupunguza vifo vya uzazi .
Ummy alisema kuwa ,watumishi na wauguzi
wengi wanajituma na kufanya kazi zao kifanisi ila wapo wachache ambao
wanakwamisha juhudi hizo .
"Sitokubali mtumishi anakwenda kinyume
na serikali ,rais wetu John Magufuli anasisimamia suala zima la
kuboresha huduma za afya ,halafu akitokea mtu mmoja mzembe
anatuchanganya kwakweli sitoweza kumfumbia macho "
"Wananchi wamekuwa waoga hata kuingia
katika suala la bima ya afya kwa sababu ya mambo kama haya ,namsimamisha
mganga mfawidhi huyo hadi hapo uchunguzi utakapokamilika ." alisema
Ummy .
Mbali ya hayo Ummy alibainisha,bajeti ya
dawa katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha imeongezeka ndani ya miaka
miwili mfululizo kwenye uongozi wa serikali ya awamu ya tano .
Ummy alisema mwaka 2015/2016 bajeti ya
madawa katika halmashauri hiyo ilikuwa mil.24 na 2017 ilifikia mil.70 na
bajeti ya sasa 2017/2018 imefikia sh. mil.101 .
Kwa upande wake mama aliyejifungua
kituoni hapo ,Salma Khalfani ,alimweleza Ummy kwamba aliandikiwa orodha
ya dawa za kununua kwenye maduka ya dawa ya nje .
Alieleza ,alitakiwa kufanyiwa upasuaji
na hivyo kutakiwa kununua madawa na vifaaa tiba ,pamba na gloves vya
180,000 akanunue ili aweze kujifungua .
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo ,Mmbaga alisema maagizo aliyopewa na waziri ameyapokea na atayafanyia kazi .
Nae mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini
,Hamoud Jumaaa alisema kumekuwa na malalamiko mengi juu ya wananchi hasa
akinamama kulipishwa fedha za dawa na vifaa tiba .
Alisema baadhi ya wazee wamekuwa wakishindwa kupewa huduma za afya bila malipo .
Jumaa alimuomba Ummy kuendelea kushirikiana nae kuwadhibiti watumishi wazembe wanaodidimiza haki za wananchi
0 comments:
Post a Comment