MWALIMU ALIYEFUMANIWA AKIFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI ASIMAMISHWA KAZI Kadama Malunde Monday, July 24, 2017

 

Mwalimu wa somo la Baiolojia katika shule ya sekondari ya wasichana ya St Therese ambaye alidakwa akifanya mapenzi na mwanafunzi katika maabara ya shule hiyo amesimamishwa kazi akisubiri hatua za kinidhamu dhidi yake.


Ofisa Elimu wa Wilaya, Christopher Sinkamba akizungumza alisema kwamba maamuzi hayo yamechukuliwa baada ya wananchi wengi kulalamika. 


Sinkamba alisema mwalimu anayehusika ametambuliwa kama Raphael Mwape na kwamba sasa anasubiri hatua za kinidhamu dhidi yake.


Alisema kwamba utawala wa shule ulifikisha suala hilo Polisi lakini walishindwa kumshtaki kwa tuhuma za kubaka kwa kuwa binti huyo ni zaidi ya miaka 16. 


Na wakati alipoulizwa swali kwanini mwanafunzi huyo wa kike ametimuliwa shule, ofisa huyo alisema kwamba hawajamfukuza lakini walilazimika kumhamisha shule kutokana na sheria za shule hiyo.


Ilielezwa kuwa tukio hilo lilifanyika saa 12 jioni ambapo Mwape alionwa na mabinti wengine wawili wa shule hiyo akifanya mapenzi na binti huyo katika maabara B ya shule hiyo. 


Mwanafunzi huyo alisema kwamba hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa mwalimu huyo kumuingilia na kwamba siku hiyo alilazimika kufanya hivyo baada ya kushinikizwa na mwalimu aliyemuita wakati akirejea bwenini.


Alisema pamoja na kukataa kwake alimshinikiza kwa kudai kuwa alikuwa amemgharamia sana. Mwalimu huyo ana mke.

Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment