Hospitali mpya ya mkoa kujengwa mkoani Rukwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven

SERIKALI inatarajia kujenga hospitali mpya ya rufaa ya mkoa wa Rukwa ili kupunguza msongomano wa wagonjwa katika hospitali ya sasa ya mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven, amesema hospitali ya sasa ya mkoa, inaelemewa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaofi ka kutibiwa. Zelothe alieleza tayari eneo la ardhi kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo mpya, limepatikana na fi dia imeshatolewa kwa wananchi ili kupisha ujenzi wake.
Alisema hayo alipozindua huduma ya madaktari bingwa chini ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), walioletwa mkoani Rukwa kutoa huduma mbalimbali kwa wagonjwa kuanzia Julai 3 hadi 8, mwaka huu .
Madaktari bingwa saba watatoa matibabu ya kibingwa kwa magonjwa mbalimbali yakiwemo ya watoto, wanawake na mfumo wa uzazi, mfumo wa mkojo, mfumo wa pua , koo masikio na magonjwa ya moyo na ya ndani. Hafl a hiyo ilifanyika viwanja vya Hospitali ya mkoa wa Rukwa mjini Sumbawanga.
Share on Google Plus

About KAPOLA NEWZ TV..✍️

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment