- 118, malawi 8, burundi 13 na botswana 1. pia magari 3 yalikamatwa yakisafirisha wahamiaji haramu hao ambayo ni t. 347 daj toyota haice, t. 917 awm aina ya fuso na t.155 azu aina ya isuzu canter pamoja na wasafirishaji 7 watanzania wamefikishwa mahakamani pamoja na magari hayo.
- Pombe kali zilizopigwa marufuku na serikali zenye vifungashio vya plastiki zenye thamani ya zaidi ya tshs 1,023,508, 750/= zilikamatwa maeneo mbalimbali mkoani mbeya na kuzuiliwa kusubiri maelekezo toka serikalini.
Baadhi ya matukio makubwa yaliripotiwa kutokea ikiwemo mauaji, kubaka, unyang’anyi na uvunjaji.
Jumla ya makosa yote ya jinai yaliyoripotiwa katika kipindi cha januari hadi juni – 2017 yalikuwa ni 12,108 ikilinganishwa na makosa 11,967 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho mwaka 2016, hivyo kuna ongezeko la makosa 141, sawa na aslimia 1.
Kati ya makosa hayo, makosa makubwa yalikuwa 1, 037 wakati kipindi kama hicho mwaka 2016 makosa makubwa yalikuwa 1,040, hivyo kuna pungufu ya makosa 3, sawa na aslimia 0.2. Aidha katika kipindi hicho cha januari hadi juni – 2017 makosa madogo yaliyoripotiwa 11,071 wakati kipindi kama hicho mwaka 2016 yalikuwa 10,927, hivyo kuna ongezeko la makosa 144, sawa na asilimia 1.
Makosa yatokanayo na jitihada za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine kupitia misako/doria kwa kipindi cha januari hadi juni – 2017 yalikuwa 323 wakati kipindi kama hicho mwaka 2016 yalikuwa 305, hivvyo kuna ongezeko la makosa 18, sawa na asilimia 6.
Kwa upande wa makosa ya usalama barabarani, jumla ya makosa yote ya ajali pamoja na yale ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na usafirishaji kwa kipindi cha januari hadi juni – 2017 yalikuwa 36,930, wakati kipindi kama hicho mwaka – 2016 makosa 33,533 yaliripotiwa.
Matukio ya ajali kwa kipindi cha januari hadi juni – 2017 yalikuwa 78, wakati kipindi kama hicho mwaka 2016 yalikuwa 184, hivyo kuna pungufu ya makosa 106, sawa na asilimia 58.
Ajali zilizosababisha vifo kwa kipindi cha januari hadi juni 2017 zilikuwa 44, wakati kipindi kama hicho mwaka 2016 ziliripotiwa ajali 80, hivyo kuna pungufu ya makosa 36, sawa na asilimia 45.
Watu waliokufa kutokana na ajali kipindi cha januari hadi juni – 2017 walikuwa 53, wakati kipindi kama hicho mwaka 2016 walikufa watu 95, hivyo kuna pungufu ya watu 42, sawa na asilimia 44.
Ajali za majeruhi kwa kipindi cha januari hadi juni – 2017 zilikuwa 34, wakati kipindi kama hicho mwaka 2016 ziliripotiwa ajali 104, hivyo kuna pungufu ya ajali 70, sawa na asilimia 67.
Watu waliojeruhiwa katika ajali mbalimbali kwa kipindi cha januari hadi juni – 2017 walikuwa 67, wakati kipindi kama hicho mwaka 2016 walikuwa watu 248, hivyo kuna pungufu ya watu 181, sawa na asilimia 73.
Pesa zilizokusanywa kutokana na makosa mbalimbali ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na usafirishaji [notification] kwa kipindi cha januari hadi juni – 2017 zilikuwa Shilingi za Kitanzania 1,107,900,000/= wakati kipindi kama hicho mwaka 2016 zilikusanywa pesa Shilingi za Kitanzania 1,005,990,000/=, hivyo kuna ongezeko la tozo Shilingi 101,910,000/=, sawa na asilimia 10.
Zipo baadhi ya sababu zilizopelekea kuongezeka kwa matukio ya ajali za barabarani ambazo ni:- kuongezeka kwa vyombo vya usafiri mkoani mbeya hasa magari na pikipiki, baadhi ya madereva kutokuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na mwendo kasi hasa usiku na ulevi licha ya jitihada za Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na baadhi ya wadau kutoa elimu hiyo mara kwa mara pamoja na hali ya hewa hususani ukungu na utelezi katika baadhi ya maeneo ya barabara ya Mbeya/Rungwe/Kyela.
WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi Dhahiri A. Kidavashari anatoa pongezi kwa wananchi wote wa mkoa wa Mbeya kwa ushirikiano wao wa dhati kwa Jeshi la Polisi katika mapambano dhidi ya uhalifu na wahalifu kupitia dhana ya ulinzi shirikishi na polisi jamii katika kipindi chote cha januari hadi juni – 2017, aidha anatoa rai kwa jamii kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika mapambano dhidi ya uhalifu na wahalifu kwa kuwafichua wahalifu kwani wanaishi nao katika jamii.
Aidha Kamanda Kidavashari anatoa wito kwa jamii hasa wahalifu kuacha tabia yakuwa na tamaa ya utajiri wa haraka kwa kujipatia utajiri wa haraka kwa njia ya mkato/haramu badala yake wajishughulishe kwa kufanya kazi halali na kupata kipato halali kwa kuzingatia kuwa Mkoa wa Mbeya unazo fursa nyingi ikiwa ni pamoja na hali ya hewa. amewataka pia madereva kuendesha vyombo vya moto kwa kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika kwani zinarudisha nyuma maendeleo katika jamii hususani nguvu kazi ya taifa. Kadhalika amewataka watumiaji wengine wa barabara wakiwemo watembea kwa miguu kutii na kuheshima alama za barabarani.
Pia Kamanda Kidavashari anatoa wito kwa wakulima na wafugaji kuwa makini hasa katika kipindi hiki cha msimu wa mavuno ikiwa ni pamoja na kuepuka kufanya biashara na watu wanaowatilia mashaka, kuepuka kuhifadhi fedha nyingi ndani na badala yake wakahifadhi fedha benki kwa usalama zaidi.
Imesainiwa na:
[DHAHIRI A. KIDAVASHARI – DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment